Revelation of John 17

1Mmoja wa malaika saba aliyekuwa na vitasa saba alikuja na kuniambia, “Njoo, nitakuonesha hukumu ya kahaba mkuu akaaye juu ya maji mengi, 2ambaye wafalme wa nchi wamefanya mambo ya uzinzi naye na juu ya mvinyo wa uzinzi wake wakaao duniani wameleweshwa.”

3Malaika akanichukua katika Roho mpaka nyikani, na nilimwona mwanamke amekaa juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya matukano. Mnyama alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. 4Mwanamke alivikwa nguo ya zambarau na nyekundu na amepambwa kwa dhahabu, mawe ya thamani, na lulu. Alikuwa ameshikilia mkononi mwake kikombe cha dhahabu kilichojaa vitu vya machukizo ya uchafu wa uasherati wake. 5Juu ya paji la uso wake limeandikwa jina la siri: “BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA YA VITU VYA MACHUKIZO YA NCHI.”

6Nikaona ya kuwa mwanamke huyo alikuwa amelewa kwa damu ya waumini na damu ya waliokufa kwa ajili ya Yesu. Wakati nilipomwona, nilikuwa na mshangao mkuu. 7Lakini malaika akaniambia, “Kwa nini unashangaa? Nitakueleza maana ya mwanamke na mnyama amchukuaye (mnyama huyo mwenye vichwa saba na zile pembe kumi).

8Mnyama uliyemwona alikuwepo, hayupo tena sasa, lakini yuko tayari kupanda kutoka katika shimo lisilo na mwisho. Kisha ataendelea na uharibifu. Wale wakaao juu ya nchi, wale ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu - watashangaa wamwonapo mnyama aliyekuwepo, kwamba hayupo sasa, lakini yupo karibu kuja.

9Wito huu ni kwa ajili ya akili zilizo na hekima. Vichwa saba ni milima saba ambapo mwanamke alikaa juu yake. 10Nayo pia ni wafalme saba. Wafalme watano wameanguka, mmoja yupo, na mwingine hajaja bado; wakati atakapokuja, atakaa kwa muda mfupi tu.

11Mnyama aliyekuwepo, lakini sasa hayupo, yeye pia ni mfalme wa nane; lakini ni mmoja wa wale wafalme saba, na anaenda kwenye uharibifu.

12Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao hawajapokea ufalme, lakini watapokea mamlaka kama wafalme kwa saa moja pamoja na mnyama. 13Hawa wana shauri moja, na watampa nguvu zao na mamlaka yule mnyama. 14Watafanya vita baina yao na Mwana kondoo. Lakini Mwana kondoo atawashinda kwa sababu ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme - na katika yeye tuliitwa, tulichaguliwa, waaminifu.”

15Malaika akaniambia, “Yale maji uliyoyaona, hapo alipoketi yule kahaba ni watu, makutano, mataifa na lugha.

16Zile pembe kumi ulizoziona - hizo na yule mnyama watamchukia yule kahaba. Nao watamfanya kuwa mpweke na uchi, watamla mwili wake, na watauteketeza kwa moto. 17Maana Mungu ameweka mioyoni mwao kubeba kusudi lake kwa makubaliano ya kumpa mnyama nguvu zao kumtawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia.

Yule mwanamke uliyemwona ni mji ule mkubwa utawalao juu ya wafalme wa nchi.”

18

Copyright information for SwaULB